GET /api/v0.1/hansard/entries/541345/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 541345,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/541345/?format=api",
"text_counter": 163,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 751,
"legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
"slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
},
"content": "Asante sana, Mhe. Naibu Mwenyekiti wa Muda. Nimesimama kuunga mkono msimamo wa Kamati ya Mazingara na Mali Ghafi. Tutakapokubaliana kuwa magavana hawawezi kukaa katika bodi hii ambayo ni bodi kuu inayosimamia mipangilio ya Serikali, itakuwa ni kama tumemfungulia mlango mtu atakayekuja kubadilisha mipangilio iende sawa na kule kwake anakotawala. Kwa hivyo, kama kweli zile kamati ambazo zinasimamia mambo ya mazingira katika maeneo ya kaunti watahitaji neno lolote, kuna mwandishi ambaye ni mwakilishi wa Serikali Kuu. Kama wana neno, litapitishwa mpaka lifike kwa hii Bodi kuu kupitia kwa huyo mwandishi. Lakini kukaa katika hii Bodi itakuwa ni kama kwamba tumetoa nafasi wao waje waanze kuingilia mpangilio ambao ni wa Serikali Kuu. Hiyo itakuwa kinyume cha Katiba."
}