GET /api/v0.1/hansard/entries/541977/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 541977,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/541977/?format=api",
"text_counter": 249,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Nassir",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2433,
"legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
"slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
},
"content": "Mwaka uliopita, nilizuru viwanda ambavyo vinasafisha na kuweka samaki katika mikebe. Nilisikitika kuona kuwa idadi ya watu waliokuwa wameajiriwa kwenye kiwanda hicho ilikuwa ni ndogo sana, na hali Wakenya huenda kwenye nchi kama vile Ushelisheli ili kupata ajira katika sekta ya uvuaji samaki. Sababu kuu ni kwamba nchi nyingine zimeweka sheria kuhusu uvuaji wa samaki. Uvuaji wa samaki ni shughuli ambayo huziletea nchi nyingi ulimwenguni dola kwa mabilioni. Jambo la kusikitisha ni kwamba, katika nchi hii, mwenye meli yake anaweza kuingia na akiweza kulipa dola elfu hamsini, anaweza kuvua samaki wanaoweza kujaa meli yake. Wengine huvua mpaka meli zao zikafikia “kutapika”. Kuhusu jambo hilo, hamna lolote linalowasaidia Wakenya, na hususan wale wanaotoka kwenye sehemu ambazo zina ufuo wa bahari au mito. Ningependa kutaja kwa kibinafsi na kwa niaba ya watu wa Mvita, kwmba tunaukubali Mswada huu kwa sababu unaweka mpangilio katika sekta ya uvuvi, na kuangalia ni chombo gani kinachofaa na ni kipi ambacho hakifai kwa sababu kinaharibu mandhari ya bahari, ama kinasababisha samaki kufa kwa wingi. Pia njia itakayotumiwa na vyombo vya uvuaji vitakavyotumika, italeta uchafuzi wa bahari na mambo mengine ambayo sheria hii itasaidia. Kando na kuvua samaki tanaowajua wa kawaida, sheria hii imeweza kuongeza maswala ya ufugaji wa samaki, na sio uvuvi wa samaki tu. Kitu ambacho ningeomba, na nimeweza kudokezea wenzangu hapa, ni kuwa sheria ikiwa na nia na madhumuni mazuri, tusiichafue kwa sababu ya hali ya kisiasa. Huu Mswada imeweka bodi tatu, nazo ni Kenya Fisheries Council, Kenya Fisheries Service na Fish Marketing Authority. Katika yale ambayo ninayapinga ni kuwa bodi hizi zimeambiwa ofisi zao kuu ziwe Nairobi. Ingawa nina uchache wa elimu, ingawa nilipata alama ya “A” katika Jiografia, sikumbuki kuwa Nairobi ina mto wala bahari. Itakuwa sawa kwa wale wamejaliwa na kubarikiwa na raslimali hii, makao makuu ya bodi hizi yawe mapahali ambapo uvuvi unafanyika. Imesekana kuwa Mswada huu hauhusishi serikali za kaunti. Ukifika katika Seneti, wenzetu wanaweza kuipigia fujo. Ningependa tukumbushane kwamba katika Orodha ya Nne ya Katiba ya Kenya, kifungu cha kwanza kinaipatia Serikali kuu uwezo juu ya maswala ya kulinda mandhari na hali vile ilivyo kuhusiana na mambo ya uvuvi, uwindaji na ukulima. Lakini swala la ukulima, hususan tukizungumzia mambo ya samaki, katika Katiba ya Kenya ni wazi kuwa ni jukumu la serikali za kaunti. Kwa hivyo tusibuni sheria ambayo italeta siasa. Ningeomba Serikali iyakumbatie maswala ya ugatuzi na wale wanaoendesha serikali za kauti; infaa huu Mswada upitie Seneti ili kila mmoja aukubali. Ningeomba Wabunge wenzangu ambao wana mito, ziwa ama bahari, na wale ambao, kwa sababu pengine wana kuku na ngamia peke yake, waingilie ufugaji amaki; he wainzingatia sheria hii, wakae chini na serikali zao za kaunti na wavuvi katika maeneo yao ili tukitengeneza sheria iwe ni sheria ambayo itafaidi wakenya wote. Asante sana, Naibu Spika wa Muda, kwa nafasi hii."
}