GET /api/v0.1/hansard/entries/542031/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 542031,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/542031/?format=api",
"text_counter": 41,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Kombe",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 250,
"legal_name": "Harrison Garama Kombe",
"slug": "harrison-kombe"
},
"content": "Ahsante Mhe. Spika kwa kunipa fursa hii ili nami nichangie Mswada huu. Kwanza, ningependa kumpongeza mhe Odhiambo-Mabona kwa kujifikiria yeye mwenyewe na wengine ambao hawana uwezo wa kupata mimba. Hivyo, Mswada huu ukiwa sheria, utawasaidia wale tasa kupata watoto kwa kutumia njia ya yai kutoka kwa mtu mwingine likichanganywa na mbegu za kiume kisha kuweza kuwekwa katika tumbo lake. Kwa hakika, wengi huwa wanagadhabika kwa kutopata watoto, hasa akina mama. Kama tunavyofahamu, wakati mwingi watu huwa katika hali ya kuwafyolea wale wengine wasiokuwa na uwezo wa kupata watoto. Watoto ni Baraka kutoka kwa Mungu, na ndiyo maana wakati wote tuna wachukua watoto kama wasaidizi wetu. Vile vile, tunajivunia kwamba wao ndio viongozi wa kesho. Ijapokuwa mara nyingi wengi walio mamlakani husema vijana ndio viongozi wa kesho, hiyo kesho huwa haifiki. Hata hivyo, ni jambo la busara. Ningehimiza wenzangu waunge mkono zaidi Mswada huu. Utakapofika katika kamati, itafaa tuweze kufanya mabadiliko yatakayozidi kuongezea nguvu sheria hii. Kwa hayo machache, naunga mkono."
}