GET /api/v0.1/hansard/entries/542962/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 542962,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/542962/?format=api",
"text_counter": 21,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Kombe",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 250,
"legal_name": "Harrison Garama Kombe",
"slug": "harrison-kombe"
},
"content": "Kwa haraka, nitapitia suala la Katiba. Sio wengi walipata kuifahamu Katiba. Kwa haraka tuliipitia na kuipitisha. Laiti wangejua yale madhara ambayo yangewakumba kama yanavyotukumba siku ya leo, Katiba hatungeipitisha kamwe. Tungeisimamisha, tuirekebishe kisha tuipitishe. Miezi michache iliyopita katika sehemu za magharibi ya nchi hii, kuna bunge lililopitisha kwamba watu ambao wamefuga kuku na paka watozwe ushuru. Watu walilalamika ilhali wao walikuwa wanatekeleza yaliyomo katika Katiba. Vile vile, walipitisha Katiba bila kufahamu kwamba nyumba wanazolala ndani zitatozwa kodi. Hilo likitendeka nina hakika Wakenya wote watalalamika. Hivyo basi kuna umuhimu sana wa kuhakikisha kwamba Katiba na sheria zote za nchi zinatafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili na kwa lugha nyepesi. Nikiwa mtaalamu wa lugha hii ya Kiswahili niko tayari kushughulika katika harakati hiyo ya kutafsiri Katiba na pia sheria za nchi. Naunga mkono."
}