GET /api/v0.1/hansard/entries/542966/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 542966,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/542966/?format=api",
"text_counter": 25,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwashetani",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2163,
"legal_name": "Khatib Abdallah Mwashetani",
"slug": "khatib-abdallah-mwashetani"
},
"content": "hawa watoto wanapoitwa kuhojiwa ili kupata kazi. Wengi wanakosa kazi kwa sababu wameshindwa kujieleza kwa lugha ya Kiingereza ilhali wamesoma, wako na stakabadhi na wamepita. Ndiposa unaona inakuwa shida kwa watoto wetu kupata kazi haswa katika Serikali na sehemu zingine ambazo si za Serikali. Wale wanaowakilisha nchi yetu ya Kenya kama Mabalozi kutoka Ulaya na Uingereza, kabla hawajatumwa hapa, ni aula kwao kufundishwa ama kujifundisha lugha ya Kiswahili ili wakija hapa waweze kuwasiliana na wakaaji wa nchi yetu ya Kenya. Lugha ya Kiswahili inatambulika katika Afrika Mashariki. Ikiwa tutaendelea katika Muungano wa Afrika Mashariki, itakuwa muhimu kuitambua lugha ya Kiswahili na tuipatie kipao mbele ili iwe katika zile lugha ambazo zinasikika. Mbali na Kiingereza, Kiswahili iwe lugha ya pili au ya tatu. Hii ni lugha ambayo inatambulika katika eneo kubwa. Naunga mkono Hoja hii.Tukiipitisha, tutaleta Mswada hapa Bungeni ambao utawafaa Wakenya wengi."
}