GET /api/v0.1/hansard/entries/542967/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 542967,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/542967/?format=api",
"text_counter": 26,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Letimalo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 68,
"legal_name": "Raphael Lakalei Letimalo",
"slug": "raphael-letimalo"
},
"content": "Nakushukuru, Mhe. Naibu Spika kwa kunipa nafasi hii ili nami niichangie Hoja hii. Ni wazi kwamba lugha ya Kiswahili inatumika wakati wowote. Inatumika ofisini, katika biashara, kwa mashule na sehemu zinginezo. Haka kama mtu hakuhitimu kwa masomo, bado anaifahamu lugha ya Kiswahili kuliko Kiingereza. Kwa hivyo, ni muhimu tuitafsiri Katiba yetu na sheria zingine ili Wakenya wote wafaidike. Katiba yetu inasema kwamba ni lazima wananchi wahusishwe katika mipango yote ambayo inawahusu. Kwa hivyo, Bunge ina sababu ya kuwahusisha wananchi kama tunavyosema katika Kiingereza, public participation . Inakuwa muhimu kwa wananchi kutoa maoni yao. Lakini kwa sababu haya yote yameandikwa katika lugha ya Kiingereza, inakuwa ni vigumu sana kwa wananchi, hata ikiwa wangekuwa na maoni, kuyatoa. Ni vyema, hasa katika sehemu zingine ambapo masomo yako katika hali ya chini ili wananchi kutoka sehemu hizo wahusishwe. Ukiangalia maadili au sera za Serikali, zote zinatoka katika Katiba. Wale ambao wanahusika, kama vile maafisa wa Serikali na viongozi wa siasa, wanatumia mikutano ya hadhara kuelimisha wananchi. Inakuwa vigumu ikiwa kila kitu kitahitaji kutafsiriwa ili ilete usawa. Kama Katiba imeandikwa kwa lugha ya Kiswahili, itakuwa rahisi kuwaelimisha wananchi ili waelewe wajibu wao. La mwisho, ambalo mara kwa mara linakuwa tatizo na kama vile mwenzangu amesema, mshtakiwa anapelekwa kortini, mashtaka yote yameandikwa kwa lugha ya Kiingereza na haelewi Kiingereza na wakati mwingine, Kiswahili chake ni duni. Inabidi huyo mshtakiwa kufungiwa hadi wakati korti litapata mtu ambaye ataweza kutafsiri kwa lugha ambayo mshtakiwa anaelewa. Jambo hili hutatiza. Itachukua muda mrefu kwa mshtakiwa kupata haki yake. Ni muhimu Katiba yetu na sheria zote zitafsiriwe kwa lugha ya Kiswahili ili wananchi wafaidike."
}