GET /api/v0.1/hansard/entries/543652/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 543652,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/543652/?format=api",
    "text_counter": 480,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Shaban",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": "Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda. Mimi pia ningetaka kujiunga na wenzangu kutuma risala zangu za rambi rambi kwa wapendwa wote ambao wamepoteza watoto wao. Ni jambo la kusikitisha sana kwamba miaka 52 baada ya kupata Uhuru, watoto wetu wanauawa kama kwamba maisha hayana umuhimu. Pale tumefikia sasa, inatubidi tukae pamoja sote tukubaliane kwamba tatizo lipo, na kwamba ni lazima tatizo hili tulitatue. Wale ambao walifiliwa ni wazazi. Watoto wao walikwenda chuoni kusoma kwa shida. Kulingana na jinsi walivyopoteza watoto wao, siyo sawa sisi, kama Wakenya, kufikiria kwamba Kenya iko huru. Ni lazima matatizo yanayotukabili yatatuliwe. Rais na Amiri-Jeshi-Mkuu wa nchi hii anahitajika kuketi chini na viongozi wote kwa pamoja ili tuweze kulitatua tatizo hili. Ni jambo la kusikitisha kwamba mashambulizi yalipoanza saa kumi na moja asubuhi, askari wanaosimamia usalama walichelewa kwenda kuwaokoa watoto chuoni kwa sababu ya mvutano uliopo Serikalini. Ni kama kwamba watu hawafahamu kazi ambayo wanatakiwa kufanya. Niliangalia orodha ya mawaziri waliokimbilia kule ilhali The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}