GET /api/v0.1/hansard/entries/54466/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 54466,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/54466/?format=api",
"text_counter": 353,
"type": "speech",
"speaker_name": "Dr. Machage",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 179,
"legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
"slug": "wilfred-machage"
},
"content": "Kwa hivyo, tuweke akili zetu pamoja, ili tutatue tatizo hili. Ukweli ni kwamba bei na gharama ya kununua mafuta imeenda juu na hali ya maisha imekuwa ngumu. Ukweli ni kwamba Waziri alijaribu kupunguza bei ya mafuta jana kwa shilingi mbili na tunajua jambo hili. Lakini ukweli ni kwamba ni sisi wenyewe katika Bunge hili tuliweka sheria za kutoa ushuru wakati wa kuongea juu ya makadirio ya fedha za Serikali. Makosa ni yetu wote katika Jumba hili. Wengine wasijifanye kwamba hawakufanya hilo kosa. Kwa hivyo, lililoko ni sisi wenyewe tukae, tutafakari na tuiangalie Bajeti tuliyoipitisha. Je, Bajeti tuliyoipitisha na nguvu tulizompa Waziri wa Fedha zinafaa katika mazingira ambayo tumejipata wakati huu au inabidi kwamba sisi tugeuze sheria za kutoza ushuru kusudi mwananchi asiumie? Hii ni kwa sababu Waziri wa Fedha ana uwezo kidogo ambao anaweza kupunguza gharama ya mambo. Sisi ndio tunao huo uwezo na tusije tukajifanya."
}