GET /api/v0.1/hansard/entries/54472/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 54472,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/54472/?format=api",
"text_counter": 359,
"type": "speech",
"speaker_name": "Dr. Machage",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 179,
"legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
"slug": "wilfred-machage"
},
"content": "Ni heri tujaribu kuwasaidia wananchi wetu, hasa wale wamekosa chakula. Ni lazima kama Bunge hili kutafakari mbinu maalum za kuweza kuwasaidia watu wetu. Lawama hazitasaidia wananchi wetu kupata unga na baadhi nyingi za kimsingi. Ni lazima tupate suluhu ya janga hili. Mhe. Mbunge amependekeza pesa ziongezwe kwa minajili ya kununua mbegu ili wakulima waweze kupanda, ili tuepukane na njaa siku zijazo. Jambo la pili ni kuhusu ukosefu wa chakula hapa nchi. Wananchi wa sehemu yangu wana chakula za kutosha. Maghala yetu yimejaa mahindi. Kwa hivyo, ningependa Serikali itenge pesa za kutosha za kuweza kununua mahindi kutoka kwa watu wetu. Wakati huu, bei ya chakula ni ghali sana. Iwapo Serikali itanunua mahindi yetu kwa bei nafuu, basi hali ya maisha itaenda chini. Haifai Serikali kuagiza chakula kutoka nje kwa bei ya juu. Tunataka suluhisho ya janga hili ambalo limeikumba nchi yetu, wala hatutaki viongozi kulaumiana hapa na pale. Si jambo nzuri kusema fulani ameiba hapa na pale bila kutoa suluhu ya shida yetu. Sawa wameiba, lakini sasa kuna shida katika nchi hii. Taabu si kwamba mifereji ya mafuta ni midogo, au magala yetu ni madogo na kadhalika. Tabu ni kuwa wafuta tunayoyanunua kutoka nje si mengi. Je, tutapata wapi pesa ili gharama ya maisha iende chini? Je, ni wapi tunaweza kupata mafuta ya bei nafuu? Haya ndiyo maswali ambayo tunahitaji kuyajibu katika Bunge hili."
}