GET /api/v0.1/hansard/entries/546765/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 546765,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/546765/?format=api",
"text_counter": 195,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Amolo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 631,
"legal_name": "Rachel Ameso Amolo",
"slug": "rachel-ameso-amolo"
},
"content": "wetu wote wakifaulu katika shule za msingi na shule za upili. Ukisoma bila kufanya mtihani wa kitaifa, hakuna mahali popote ambapo utaelekea. Kwa hivyo, ni jambo nzuri sana tunapoona kuwa zile senti za kulipia mitihani ya kitaifa zitatolewa kabisa katika shule zetu. Utapata watoto wengi sana wamemaliza shule lakini hawawezi kupata vyeti vyao ili waweze kujiendeleza kimaisha. Waheshimiwa wenzangu, mtakubaliana nami kuwa kuna watoto wengi sana, ambao wemekaa nyumbani kwa sababu hawakuweza kulipa pesa za mtihani wa kitaifa walipokuwa shuleni. Kwa hivyo, tukiondoa pesa hizi za kulipia mtihani wa kitaifa, tutakuwa tumesaidia nyumba nyingi sana katika nchi yetu ya Kenya. Pia tutakuwa tunawasaidia watoto wengi ambao hawangekuwa viongozi kama sisi hii leo, kwa sababu ya kukosa senti za kulipia mtihani wa kitaifa, na hivyo basi kukosa kufaulu kimaisha. Kwa hivyo, naunga mkono jambo hili. Naomba tutoe kabisa zile pesa zinazolipwa za kufanya mtihani wa kitaifa iwe ni darasa la nane ama kidato cha nne. Katika sekta ya elimu ni kuwa tulielezwa vizuri sana kwamba walimu wakuu wangepeane vyeti. Lakini mpaka wa sasa watoto wakienda shuleni wanaelezwa ni lazima walipe pesa kabla ya kupewa vyeti vyao. Ningeomba kwamba tuwe na sheria, ili walimu wakuu wapeane vyeti vya wanafunzi waliomaliza kusoma ili wajiendeleze katika maisha yao. Sheria inapopitishwa Bungeni, ni lazima ifuatwe. Kuna sheria nyingi ambazo tumepitisha hapa Bungeni lakini bado hazijaanza kufuatwa. Ninaomba walimu wakuu popote pale walipo wawapatie watoto vyeti vyao ili waweze kujiendeleza kimaisha, na wajiunge na vituo mbali mbali. Hivi majuzi mliona polisi wakisajiliwa. Ingawa hivyo, watoto wengi hawakuweza kujiwasilisha kwa usajili huo kwa sababu hawakuwa na vyeti vya kudhibitisha kuwa wamehitimu katika kidato cha nne. Naunga mkono Mswada huu. Naomba walimu watilie mkazo kuona kwamba watoto wetu wanapata vyeti ili wajiendeleze kimaisha. Ahsante sana mhesh. Naibu Spika wa Muda."
}