GET /api/v0.1/hansard/entries/546823/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 546823,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/546823/?format=api",
"text_counter": 253,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Katana",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 691,
"legal_name": "Aisha Jumwa Katana",
"slug": "aisha-jumwa-katana"
},
"content": "Mhe. Naibu Spika wa Muda, nataka kusema kwamba nimesimama kuunga mkono kabisa Mswada huu ambao utakuwa muhimu kwa sababu tumeona Rais wa Jamhuri ya Kenya akitoa amri kwamba malipo ya mitihani yetu ya kitaifa ya Darasa la Nane na Kidato cha Nne yote yaondolewe. Serikali imejitolea kabisa tukipitisha Mswada huu itakuwa ni sheria, na itakuwa ikifanyika bila pingamizi. Hii ni kwa sababu Rais akiongea, ama wakuu wetu wakiongea, ni kwamba bado kuna waalimu ambao ni wakuu wa shule wanaosembea. Kwa mfano, mwaka jana tulimwona Rais wetu pamoja na makamu wetu wakiongea kuhusu vyeti vya watoto wa Kidato cha Nne, kwamba vyote vipeanwe. Tuna ushahidi kama viongozi wa kule chini nyanjani kwamba waalimu wakuu wengi wamekataa kupeana stakabadhi zile muhimu kwa watoto wetu wa Kidato cha Nne. Kwa hivyo, nataka kusema kwamba ni Mswada muhimu sana, na utasaidia The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}