GET /api/v0.1/hansard/entries/546846/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 546846,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/546846/?format=api",
    "text_counter": 276,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": "Ahsante sana Naibu Spika kwa kunipatia nafasi hii kuunga mkono Mswada huu. Kwanza napenda kumpa kongole mhe Wangwe kwa sababu ya kuleta Mswada huu. Katika nchi yetu tunaelewa kwamba jambo lolote likifanywa kisheria, linaweza kutekelezwa, na hivyo basi kuona limetendeka kwa njia inayofaa. Ni haki ya kimsingi kwa kila mtoto wa Kenya kupata elimu yenye manufaa. Jambo hili limesisitizwa katika Kifungu 42 cha Katiba yetu. Elimu yenye manufaa ni elimu ambayo mwanafunzi amesoma na baada ya kusoma ameweza kutahiniwa na baadaye kuweza kuendelea katika daraja ya pili ya kielimu. Kwa mfano, watoto wetu wengi sana hapa Kenya huweza kusoma katika shule ya msingi na wanapofika Darasa la Nane wanashindwa kulipa pesa za mtihani. Hivyo basi wanashindwa kuendelea katika masomo ya shule ya upili. Hii ndiyo sababu tunaona watoto wengi sana wanafika Darasa la Nane, lakini wanakosa kwenda katika shule ya upili. Kuhusu kuondoa umaskini, elimu ndio jambo ambalo litaweza kutuondolea umaskini katika nchi yetu ya Kenya. Ili kuondoa umaskini, lazima tuweze kupata elimu yenye manufaa na kuendelea. Mwanafunzi hawezi kuendelea kufika hata chuo kikuu ama kuenda katika shule ya kitaaluma ikiwa hajapata vyeti katika Darasa la Nane, na Kidato cha Nne. Hivyo basi tunapoteza watoto wengi wenye talanta kwa sababu wamekosa vyeti. Leo hii unapokwenda kuajiriwa katika vikosi vyetu vya ulinzi kama Jeshi la Navy ama jeshi la nchi kavu, utaulizwa cheti cha Kidato cha Nne. Iwapo hukuweza kutahiniwa na kupata cheti hicho, basi wewe huwezi kupata kazi kama hiyo. Hili ni wazo nzuri sana kwa sababu wakati tunasema elimu ni bure yatupasa tujiulize, je, kutahiniwa ikiwa hakutakuwa bila malipo tutawezaje kusema kwamba elimu imetufaidi? Rais wetu amezungumzia sana suala hili na ametangaza kwamba elimu iwe bure ili tuweze kubadilisha nchi yetu. Hii ni kwa sababu nchi nyingi zilizoendelea katika ulimwengu ni kwa sababu elimu ya upili na msingi imefanywa kuwa bila malipo. Aidha wanafunzi hawatozwi pesa za kutahiniwa. Wizara ya Elimu na ile ya Fedha, zikishirikiana na Kamati yetu ya Bajeti na Kamati ya Elimu, zihakikishe kwamba ikiwa sheria hii imepita tumeweka pesa za kutosha ambazo zitafidia pesa zile ambazo wazazi sasa watakuwa hawalipi."
}