GET /api/v0.1/hansard/entries/546857/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 546857,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/546857/?format=api",
"text_counter": 287,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Wekesa",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2742,
"legal_name": "David Wafula Wekesa",
"slug": "david-wafula-wekesa"
},
"content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika kwa kunipatia fursa hii. Ningependa kuitumia nafasi hii kumpa mheshimiwa mwenzangu heko kwa kuuleta Mswada huu. Sisi sote tunajua umuhimu wa masomo na kufanya mtihani. Ni heri sisi kama Bunge tuuhalalishe Mswada huu ili wazazi na wanafunzi wetu wajue kwamba mitihani ni ya bure. Ingekuwa muhimu pia kama wanafunzi wote wangehusishwa. Sisi sote tunaujua umuhimu wa shule za binafsi. Shule za binafsi zimechangia pakubwa sana kwa masomo hapa nchini. Tunajua kwamba shule za Serikali haziko kila mahali katika Kenya. Kuna sehemu ambazo utakuta kuna shule nne tu za sekondari za Serikali."
}