GET /api/v0.1/hansard/entries/549024/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 549024,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/549024/?format=api",
    "text_counter": 147,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 751,
        "legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
        "slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
    },
    "content": "Kwa hivyo, katika mradi huu, tuzidi kuangazia vile ambavyo tutaweza kuweka mikakati ambayo itafanya bei ya mafuta iache kupanda kila mara. Hata inaposhuka katika soko ya ulimwengu, tubaki na ile bei ambayo sisi wenyewe tunaweza kuihimili na inaweza kumsaidia mwanchi wa kawaida. Pia, tuwe waangalifu tunapojenga huu mfereji. Je, huu mradi wetu ambao ndio mradi mkuu katika eneo letu la Pwani na unasimamia Kenya nzima ambao ni Kenya Refinery, ni vipi ambavyo tunaweza kuifufua Kenya Refenery ili iwe ndio chanzo cha kuwa na mahala pa kuweka mafuta yetu kuliko vile ilivyo wakati huu? Ule mradi mkuu wa refinery umekufa na watu wengi wameachishwa kazi."
}