GET /api/v0.1/hansard/entries/549420/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 549420,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/549420/?format=api",
"text_counter": 218,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "kupunguza tu makali ya malaria lakini si kutibu. Huo ndio ukweli wa mambo. Ufurahi ama ukasirike, ukweli ni huo. Bi. Spika wa Muda, naunga mkono Mswada huu. Seneti, kama alivyosema Sen. Musila, kinagaubaga ndio waliochimbia kaburi hili tulimo. Amekubali mwenyewe hapa. Amesema kwamba walipokuwa Naivasha, walifikiria ya kwamba hili litakuwa Bunge la Wazee. Hivyo sivyo ilivyo. Kifungu 96 kwenye Katiba kimeeleza kinagaubaga kazi ya Seneti. Mwananchi anaelewa ya kwamba Seneta ni kama Mbunge wa Bunge la Kitaifa. Hizi ni fikra za mwananchi. Kwa muda wa miaka 50, wananchi wamekuwa na fikra hizo. Mpaka leo, mawazo yao hayajabadilika kwamba Seneti ndio mlinzi wa ugatuzi. Fikra zao ni zile zile. Kaunti nzima inaweza kuwa na Wabunge wanne. Wewe Seneta mmoja huna fedha za kufanyia kazi katika sehemu hiyo. Hata hivyo, unaambiwa kuwa wewe ndiye msimamizi wa rasilimali. Unatakiwa kuchunguza rasilimali ambazo fedha zinazochukuliwa zinapewa serikali ya ugatuzi ambayo inaongozwa na gavana. Kama twataka ugatuzi uonekane kwa nguvu, lazima Seneti ionekane kuwa na nguvu. Bila Seneti kuwa na nguvu, kama ulivyosema na hawa wengine wote wanaokubaliana nawe, hatutakuwa tumefanya kazi yoyote. Hii ni kwa sababu hali ilivyo sasa, mwananchi kule chini anaona gavana akifanya kazi. Gavana akifika mahali, anatoa ambulensi na bursary . Gavana akifika mahali popote, anasema kuwa; “Mimi na serikali yangu, serikali yangu imetoa bursary, serikali yangu imetoa vitu vingi.” Hakuna mahali Seneta atatajwa. Gavana akiandamana na MCAs, kila MCA anayesimama humsifu gavana kutoka wa kwanza mpaka wa mwisho ilhali wewe uko hapo hapo umeketi. Hatujulikani. Bi. Spika wa Muda, kwa kupata nyenzo, tunaweza kufanya kazi kusudi tusiwe kama wale watu wa kuitikia; “Amina” baada ya kuwa maombi yameshafanyika. Kazi yako isikuwe tu kuitikia “Amina” kama kasisi ama mwalimu wa dini ameshasoma dua yote. Bi. Spika wa Muda, kwa maoni na fikra zangu naona kwamba Mswada huu umekuja wakati mzuri. Hata hivyo, nasisitiza kwamba muda ule ambao kila kitu kinachopitishwa katika Jumba hili mpaka kirudi katika Bunge la Kitaifa, kwa neno lijulikanalo kama “concurrence” katika Kiingereza umepita. Huu utakuwa mtihani kwa sababu hakuna jambo hata moja linalokwenda katika Bunge la Kitaifa kutoka Seneti ambalo litakubaliwa na Wabunge wa Bunge la Kitaifa. Kwa mfano, hivi sasa, Mswada ambao umetoka hapa na mabadiliko machache ya Kshs7 billion mpaka sasa umekuwa na mvutano. Kamati iliyoundwa ambayo ni ya uwiano haijapata jibu hadi sasa. Haya ndiyo maswala ambayo yanaleta utata. Hili ndilo swala ambalo tunaona ya kwamba ni kuifanya Seneti ionekane ya kwamba haina kazi. Watu wengine wamekuwa na fikra kuwa Seneti iondolewe; Kuiondoa Seneti ni kuuwa ugatuzi. Nawaomba wenzangu kutoka Jubilee wasikie tunavyosema, “Okoa Kenya.” Haya tunayasema kila siku. Kenya itaokolewa hivyo. Kuiokoa Kenya ni kubadilisha hii Katiba. Kuna vipengele vinavyo tuumiza. Tunasema kuwa tuwe na majadiliano. Ya nini tuwe na majadiliano ilhali dawa ya malaria ni quinine? Kinacho takikana kufanya ni kubadilisha The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}