GET /api/v0.1/hansard/entries/550381/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 550381,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/550381/?format=api",
    "text_counter": 237,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Bule",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1029,
        "legal_name": "Ali Abdi Bule",
        "slug": "ali-abdi-bule"
    },
    "content": "Bw. Spika, jambo ambalo limetajwa hapa na Sen. Hassan, Seneta wa Kaunti ya Mombasa, ni muhimu; swala la afya katika kaunti zetu. Tunapinga yeyote yule anayetaka kuingilia swala hilo. Awali tulikuwa na matatizo hapa na pale katika sekta ya afya. Leo hii, katika kaunti zetu, akina mama wanapata huduma za afya karibu na nyumbani. Kuna vituo vya afya na hospitali kila mahali. Matatizo ya watoto kufa mapema na akina mama kukosa huduma wakiwa wajawazito hayapo tena. Bw. Spika, tunapinga yeyote yule ambaye anaingilia jambo hili. Hatutarudi nyuma bali tunaendelea mbele. Ugatuzi upo na utaendelea."
}