GET /api/v0.1/hansard/entries/550449/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 550449,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/550449/?format=api",
"text_counter": 305,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "wa mwisho. Wametangaza hadharani kwa ulimwengu mzima bila kujua kwamba walicholifanya kina madhara. Hawakuziweka sababu zao za kufanya hivyo hadharani; kinaga ubaga, kusudi wananchi wajue kwamba wametumia mbinu Fulani. Ni mbinu gani walitumia kutengeneza orodha hiyo? Lakini nikiangalia orodha hiyo bila kuingilia nafsi ya mtu au kiongozi mwenzangu, sio lazima Seneta aonekane kwamba yeye ni mtu wa kuanzisha vita mahali popote pale ili awe nambari moja. Itabainika kwamba lazima Seneta labda awe na uwezo wa kutengeneza hela zingine za tashwishi kusudi awe na miradi ambayo hata Serikali kuu haiwezi ili aonekane kwamba yeye ni nambari moja. Pengine anafaa kuwa na desturi zisizokubalika kusudi awe kati ya wakubwa kumi. Pengine anafaa kutohudhuria vikao vya Seneti. Ati usipohudhuria vikao vya Seneti, wewe waorodheshwa kuwa nambari moja. Jameni, mbiu ya mgambo hiyo! Nawatangazia wananchi kwamba, wazisome sera za kila Seneta hasa wale walioorodheshwa kuwa wa kwanza kumi; wazisome sera zao. Sisemi kwa ubaya lakini kwa sababu mkia ulikatwa, lazima ulie kwa sababu wadondosha damu. Wasome pia sera za wale ambao kila wakati wanaketi ndani ya Seneti wakipendekeza vilio vya wananchi kutoka sehemu zao na wako hapa. Wengine hata wameangaliwa na Seneti na kupewa majukumu ya kuongoza vikao vya Seneti wakiwa Seneta wa kawaida. Wamepewa majukumu ya kumsaidia Bw. Spika; ati anaorodheshwa huku nyuma. Jameni ukistaajabu ya Musa, utaona ya Firauni! Mimi siungi mkono kwamba gazeti la Daily Nation, likatazwe kuandika mambo ya Seneti kwa sababu sisi tutaonekana vibaya tukichukia hatua kama hiyo. Lakini sisi tunawaambia watahadhari wanayoyaandika. Kweli jukumu lao ni kutaka biashara, leo wameuza magazeti kwa pesa za kishindo kwa sababu ya kuwadanganya wananchi; kuwaonyesha wananchi kwamba fulani ndiye nambari moja na mwengine amevuta mkia. Sijui wameniweka wapi mimi. Nasikia niko kwenye nambari 25. Silalamiki, huenda hapo ndipo nipo. Lakini wawaangazie wananchi sababu ya kumweka huyu hapa ni gani, kusudi hata mimi nigutuke nione kwamba hili pengo lahitaji kuzibwa. Mimi sio kiongozi ambaye anataka kuona vita mashinani; kwamba mimi Seneta ati kusudi nionekane na kuorodheshwa kuwa Seneta mkuu, lazima nianzishe vita na Gavana wangu. Mimi nikiwa Seneta wa Migori, kazi yangu ni uwiano. Juzi watu wa Migori walifanya fujo na kumtupia Rais viatu; ilibidi niwakusanywe Wanamigori waje Nairobi kumwomba Rais msamaha, kwamba jambo walilofanya ni mbaya. Hiyo ndio kazi ya Seneta, kuleta uwiano na amani. Mimi kwa kweli, nisingeorodhesha Seneta yeyote anayetoka sehemu zilizo na vita ati kuwa yeye ndiye Seneta mkuu. Sehemu ambayo watu juzi wameuawa, arobaini, sitini na mia moja--- . Damu inalia kwa mikono yao. Sijataja jina la mtu lakini nimetoa mfano tu."
}