GET /api/v0.1/hansard/entries/550457/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 550457,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/550457/?format=api",
    "text_counter": 313,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Machage",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 179,
        "legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
        "slug": "wilfred-machage"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika, sio kwa kupenda kwangu lakini kwa sababu ya mfululizo wa mawazo yangu labda nikamdhuru hivyo yeyote yule anahusika. Nililosema ni kwamba tunahitaji kuwa na amani mashinani. Nilisema pia kwamba sisi viongozi tunastahili kuwa mrengo wa mbele kuhakikisha kwamba amani imedhihirika nyumbani. Tunataka waandishi wa magazeti waajibike. Wanafaa kuajibika na kuwapa Maseneta uwezo wa kutekeleza majukumu yao mashinani. Vile sheria ilivyo sasa, usipotumia mali yako, kwa mfano, kutembelea Kaunti ya Migori iliyo na Maeneo Bunge tisa, basi huwezi kufanya kazi. Mimi napata mshahara ambao unalingana na wa Mbunge ambaye anawakilisha Eneo Bunge moja. Bi. Sarah Serem anafaa kuyaangalia masilahi yetu kwa sababu hii sio haki. Seneta anastahili kupewa uwezo wa kufanya kazi yake. Kama tutapewa uwezo wa kuiba ili tuyatekeleze majukumu yetu, basi tutaanza kupanga. Ni nini kilichobaki? Hakuna kitu ambacho tunaweza kufanya. Lakini, wengine wetu ni Wakristu, au Waislamu tuliotakasika kwa injili. Hatuwezi kuiba, kuenda kutafuta biashara ya mihadarati wala kuua ndovu ili mradi tupate pesa za kwenda kutekeleza majukumu yetu mashinani. Mungu atusamehe kwa hayo. Bw. Naibu Spika, nashukuru."
}