GET /api/v0.1/hansard/entries/550660/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 550660,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/550660/?format=api",
"text_counter": 111,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Bw. Spika, Sen. Haji ni mmoja kati ya wenyeviti wa Seneti hii wanaoheshimika sana. Rekodi yake inaonyesha alivyofanya kazi. Hata katika Bunge la Kumi hatukuwa na shida naye. Kwa hivyo, ninaamini ya kwamba ataleta ripoti haraka iwezekenavyo. Bw. Spika, Wakenya ndio wengi katika mataifa jirani ya Tanzania, Uganda, Rwanda na Burundi. Ikiwa kutakuwa na madhara, Wakenya wataathirika zaidi kuliko watu kutoka mataifa mengine. Ndio maana tunasema kuwa, kwa njia yoyote, tungependa kusikia kwamba kuna usalama wa Wakenya. Tunajua kuwa watu wengi wamekufa. Masikio ya Wakenya yamezoea kusikia vifo; wawe watoto, watu wazima, maskini, watu wanaojiweza au wanafunzi. Kila kuchao, kumekuwa na habari za vifo. Hatutaki mazoea kwamba kwa sababu vifo vimeongezeka, hata vikitokea nje ya nchi, Wakenya watavumilia. Bw. Spika, tunajua yanayoendelea kule Burundi. Wananchi wa huko wana hasira."
}