GET /api/v0.1/hansard/entries/551903/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 551903,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/551903/?format=api",
"text_counter": 118,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwakulegwa",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 101,
"legal_name": "Danson Mwazo Mwakulegwa",
"slug": "danson-mwazo"
},
"content": "Bw. Spika, tunajua kwamba kazi ni za Wakenya wote lakini hizi ni kazi za vibarua na vijana zaidi ya 100 waliletwa Voi Jumatatu asubuhi, basi wananchi walipigwa na butwaa. Walishangaa kuona watu hao wamefika katika busstation na hawajui mahali pa kwenda. Walipoulizwa na wananchi, walisema wameitwa kuandikwa kazi katika mradi wa reli. Cha kushangaza ni kwamba, inasemekana waliletwa na Mbunge wao wakiwa wameambiwa wanakuja kuandikwa kazi hapo. Walisema kila mmoja alilipa Ksh1,500 ili kuandikwa kazi hiyo. Maswali ninayouliza mimi kama kiongozi wa Taita-Taveta ni kwamba, kina mama wa Taita-Taveta wamezaa vijana wengi sana; vijana ambao hawana kazi ni zaidi ya 50,000. Kwa hivyo, waliopanga njama na kula pesa za vijana na kuwaleta Voi---"
}