GET /api/v0.1/hansard/entries/551912/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 551912,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/551912/?format=api",
    "text_counter": 127,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Siku za mwizi ni arobaini. Na siku arobaini zilifika siku ya Jumatatu tuliposhika watu waliokuja kwa wingi kuchukua kazi za vibarua. Mshangao ni kwamba, vijana hawa walilipa pesa, wakadanganywa ati kuna kazi nyingi kule Voi. Sasa imeleta shida kati ya sisi, viongozi wa Kaunti ya Taita-Taveta na vijana wetu. Wanasema kwamba kazi zao zimeuzwa na kwamba watu wanaletwa ili wao wafutwe kazi. Hali kwamba kazi za wale wenye ujuzi tunasema: “Hewala! Wakenya wengine wachukue.” Lakini kazi ya kupakua na kupakia mchanga na kufagia, hata hizo pia mtu anatolewa Meru kuja kufanya kazi Voi. Huu ni uonevu wa aina gani kwa watu wa Kaunti ya Taita-Taveta? Bw. Spika, mji wa Voi ni mji ambao makabila yote 43 yanaishi. Zaidi ya nusu ya wapiga kura wa Voi ni watu kutoka bara la Kenya. Kwa hivyo, vijana wanapotaka kufanya maandamano, ndio maana natoa ombi kwanza kwa vijana, kwamba tuachieni sisi viongozi wenu. Tutazungumza na wakuu wa Standard Gauge Railway (SGR), uchunguzi utafanywa ili ijulikane ni meneja gani ambaye aliagiza vijana waletwe? Vijana hawawezi kuamka asubuhi na kupanda bas wakijua kwamba kazi ziko. Kuna mtu aliwalaghai na amefanya hivyo mara nyingi. Vile nimesema kwamba siku za mwizi ni arobaini, mwizi tutamfichua. Langu ni kuwaomba vijana watulie. Sisi viongozi na mimi kama Seneta wa vijana wa Kaunti ya Taita-Taveta nitawatetea; kwamba haki ya kazi ya vijana wa Taita-Taveta wataipata. Kama kazi zilikuwa zimezidi, tungetegemea kaunti za karibu kama vile Kwale, Kilifi na Makueni wachangie, wala sio watu kutoka zaidi ya kilomita 1,000 kuletwa pale kwa kazi za vibarua. Ombi langu ni kwamba hao vijana watulie wala wasilete shida. Sisi, viongozi, tuko, tutafanya mazungumzo na tutayakabili mambo haya."
}