GET /api/v0.1/hansard/entries/552194/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 552194,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/552194/?format=api",
"text_counter": 109,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 751,
"legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
"slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
},
"content": "Shukran, Mhe. Naibu wa Spika. Nasimama kuiunga mkono Hoja hii na kuipongeza Seneti na pia Kamati za Nyumba zote mbili kwa sababu zimeonyesha uwiano. Nina imani kuwa uwiano huu utaendelea katika Miswada yote ili tuonekane kwamba tunafanya kazi kumsimamia mwananchi apate haki yake kwa pande ya Seneti na Bunge la Taifa lenyewe. Hoja hii imefungua mlango wa ajira zaidi kwa vijana, kina mama na wenzetu waliozaliwa na ulemavu. Hili limekuwa tatizo sugu katika maeneo yetu ya Bunge. Vijana wetu hawana kazi ilhali kandarasi zinatolewa kwa watu ambao si wenyeji wa lile jimbo na watu wetu wanawachwa bila chochote cha kujishikilia. Mswada huu umekuja kwa wakati unaofaa. Pia utasimamiwa na sheria kwamba haiwezekani kwa kandarasi zote za sehemu hiyo zitolewe bila kuhusisha wenyeji. Pia imefungua njia ambayo itatuwezesha sisi pamoja na wananchi kufuatilia kwa kina zile kazi zinazofanywa kule nyanjani na kuweza kutoa maoni yetu kama kazi haifanyiki kwa njia ya kisawa. Naupongeza huu Mswada na naunga mkono kwamba tunaweza kusonga mbele. Shukrani sana."
}