GET /api/v0.1/hansard/entries/554386/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 554386,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/554386/?format=api",
    "text_counter": 323,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, ningependa kumshukuru Sen. Sijeny kwa kuleta Mswada huu katika Seneti hii. Mswada huu ni muhimu sana kwa sababu unazungumzia maswala ambayo yanahitajika katika taifa letu, haswa katika ukurasa wa 295. Nakumbuka ulileta Hoja kuhusu moja ya maswala hayo wakati Seneti ilikuwa katika Jumba la Kenyatta International Convention Centre (KICC). Hoja hiyo ilikuwa inatafuta mwenendo ambao ungeiwezesha taifa hili kuwa na hospitali za Level 5 katika kila kaunti. Jambo hilo limezingatiwa katika Mswada huu wa Sen. Sijeny. Nitaanza na kipengele cha 22. Dada yangu, Sen. Sijeny, ameangalia ni wapi kuna shida. Nimewasikiliza Maseneta ambao wamechangia Mswada huu na wamesema mambo mengi haswa kuwasaidia akina mama na kuokoa maisha ya akina mama na mama wenye akili punguani na mtoto ambaye ni mjamzito. Hayo yaliozungumziwa yanahusu kuokoa maisha. Kipengele cha 22 kinasema kwamba itakuwa ni haki ya mtoto yeyote aliyezaliwa kupata matibabu. Leo katika taifa letu, watoto wa masikini hawapati matibabu ya kutosha. Wale wanaojiweza wanalakiwa vizuri katika hospitali na kupewa matibabu. Lakini msichana masikini ambaye anapata mimba kwa bahati mbaya hapati matibabu anapofika hospitalini."
}