GET /api/v0.1/hansard/entries/554945/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 554945,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/554945/?format=api",
    "text_counter": 281,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Dr.) Shaban",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": "Ahsante sana, Mheshimiwa Naibu wa Spika. Nasimama kuiunga mkono Hoja hii ya reli. Huu ni mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mkataba huu utatuwezesha kujenga reli mpya si hapa Kenya tu, bali katika nchi jirani ambazo ni Uganda, Rwanda na Sudan Kusini. Vilevile baadaye Tanzania itajiunga na mkataba huu. Kama ilivyotajwa, sisi tumebaki nyuma. Wenzetu wote tayari wameshaukubali mkataba huu. Hivyo basi, sisi kama Wabunge wa Bunge hili la Kumi na Moja hatuna budi kukubaliana na mkataba huu ili serikali zetu zote ziweze kufanya kazi hii ya ujenzi wa reli. Kwa wale ambao tumezuru nchi mbalimbali--- Nafahamu kwamba Wabunge wote wametembelea nchi nyingi duniani. Ni jambo la kusikitisha kuwa Afrika Mashariki bado tuko nyuma. Inasemekana kwamba Uhuru ulipatikana 1963. Mimi naonelea kwamba Uhuru kamili unapatikana sasa hivi. Hii ni kwa sababu tunanuia kuendeleza hali ya usafiri katika nchi zetu ili tufikie zile nchi zilizoendelea humu duniani. Mhe. Naibu Spika, Reli ya SGR itatusaidia kubeba mizigo kwa haraka na kuondoa mizigo mingi ambayo bado inakaa pale bandarini mwetu. Pia itasaidia kuwafikishia mizigo wateja mbalimbali katika nchi mbalimbali kwa njia rahisi. Vile vile, tukikubaliana katika mkataba huu --- Natumaini hivi leo tutakubaliana nao, ili Rais wetu akiungana na wenzake, ataweza kuzungumza bila wasiwasi kwamba nchi yake imekubaliana na nchi hizo zingine kuwezesha reli hii ijengwe haraka iwezekanavyo. Itakuwa ni jambo la kufurahisha kwamba kutoka Mombasa mpaka Nairobi mtu atasafiri kwa muda wa masaa manne pekee. Siku hizi katika barabara, inakua shida kwa sababu mara nyingi tunajikuta kwenye msongamano wa magari kwa sababu ya maroli mengi yanayobeba mizigo. Naunga mkono Hoja hii ili tuweze kusonga mbele haraka iwezekanavyo pamoja na wenzetu."
}