GET /api/v0.1/hansard/entries/555065/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 555065,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/555065/?format=api",
"text_counter": 109,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 751,
"legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
"slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
},
"content": "Shukrani Mhe. Spika. Ninasimama kuunga mkono Ripoti ya hii kamati. Wakati ninaiunga mkono, ningetaka kuzungumzia maeneo tofauti ambayo kusema ukweli kutokana na huu mradi ulivyoanza na kule unapotuelekeza, ni mradi ambao utaleta mabadiliko makubwa katika uchumi wa nchi hii yetu. Kwanza, ninapongeza huu mkataba kwa sababu umetuletea uwiano baina ya nchi yetu ya Kenya na zile nchi nyingine ambazo zimeingia katika mkataba. Hii ina maana kwamba wananchi katika hizi nchi zote nne wataweza kutembeleana kwa wakati wanaotaka bila kuchelewa hapa na pale kwa sababu ya usafiri. Pili, mradi huu, ukilinganishwa na mingine ambayo Serikali imeanzisha, umeweza kukimbizwa kwa haraka. Huu mradi wa reli umetupa tamaa kubwa hata tumeanza kuona mazao ya pesa zetu kwa sababu mradi umeanza na unasonga mbele kwa haraka sana. Tatu, mradi huu ukikamilika, barabara zetu zitaokoka. Ile hali iliyo katika mabarabara yetu saa hii ni mbaya sana. Kwanza, katika usafiri, kuna ajali ambazo The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}