GET /api/v0.1/hansard/entries/555066/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 555066,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/555066/?format=api",
    "text_counter": 110,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 751,
        "legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
        "slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
    },
    "content": "zinatokana na malori pamoja na mabasi. Mwishowe ni mauti ama majeruhi wengi sana. Lakini tutakapokuwa tunatumia reli, usafiri utakuwa na usalama zaidi. Nne, usafiri wa reli utatusaidia kwa sababu ukiangalia tabia ambayo inaendelezwa na Shirika la Ndege la Kenya, utagundua kwamba shirika hilo halimsaidii mwananchi. Kwa mfano, utafika katika kiwanja cha ndege ukijua utaondoka saa fulani. Mtawekwa pale na kile mtakachosikia ni matangazo tu: “Tunawaomba msamaha.” Lakini wewe ukichelewa kwa sababu pengine ya msongamano wa magari barabarani, ukifika pale unatozwa faini. Hii inamaanisha kwamba hili Shirika haliko pale kutusaidia sisi bali wana mambo yao wenyewe ambayo wanayaendeleza. Tano, mradi huu utawawezesha wananchi na hata sisi Wabunge kufika katika maeneo yetu ya kazi haraka sana. Kwa mfano, nitaweza kulala nyumbani Kwale na niingie pale Samburu kwa sababu nitapata usafiri wangu kwa wakati. Nitaweza kuhudhuria Bunge mapema vilivyo. Hii ni tofauti na kuwa Nairobi ambapo nitakumbwa na msongamano wa magari katika barabara kuu ya kuelekea Mombasa kisha nichelewa kufika Bungeni. Mradi huu utaweza kutuondolea ufisadi kwa upande mwingine. Ukiangalia yale yanayotendeka katika maeneo yaliyo na mashine ya kupima mizani ya malori na matrela, kusema ukweli--- Tulizungumzia hili neno wakati ambapo Mhe. Birdi alileta Mswada wake hapa. Mimi binafsi nilipendekeza kwamba tuondoa maofisa wote walioko katika haya maeneo. Hii ni kwa sababu yanayotendeka pale yanatuvunja moyo sisi kama viongozi katika nchi hii ya Kenya. Serikali, kupitia kwake Rais, inajaribu kupigana na ufisadi lakini yanayotendeka pale ni maajabu. Ikiwa tutaweza kuwaondoa wale watu kule na kuweka watu wapya ambao wana malengo ya kusafisha ufisadi, tutaweza kuongoza hii nchi yetu na kupata usafiri ambao hauna matatizo mengi kama vile ilivyo leo. Kwa upande mwingine, kidogo kuna tetesi. Sisi viongozi wa Kaunti ya Kwale tumezungumzia hizi tetesi. Hii ni kwa sababu kuna neno ambalo linaendelezwa na wale waliochukua hii kandarasi na ningeomba hili neno liende katika maandishi ya Bunge. Kuna mambo ambayo yanaenda kinyume na mkataba wa hii reli upande wa wale ambao walichukua kwa sababu kumekuwa na uchimbaji wa mchanga katika bahari yetu ya Kwale. Hakuna mahali tuliketi nao wakatueleza ni kiwango gani cha mchanga watachimba na ni faida gani watu wa Kwale ama Kaunti ya Kwale itapata. Hapo mbeleni, Kenya Ports Authority (KPA) ilichimba huo mchanga na hakuna kitu mpaka leo ambacho kimeweza kumfaidisha mwananchi wa Kwale licha ya kwamba kulikuwa na maelewano baina ya KPA na wavuvi wetu wa Kwale. Hivi leo, wavuvi wa Kwale wanaishi maisha duni kwa sababu walikuwa wakitegemea uvuvi. Uvuvi umekufa kwa sababu maeneo ya samaki yote yaliharibiwa na wale waliokuwa wakichimba huo mchanga. Hakuna lolote ambalo wametufanyia. Tunaiomba Serikali, kupitia Wizara zinazohusika; Wizara ya Mazingira na Wizara ya Usafiri, ipange mkutano ili tukae pamoja tujue mambo hayo. Tunashukuru kwa sababu mnamo Mwezi wa 11 mwaka jana, hiyo meli ilisimamishwa. Lakini hatujui bado kutatokea kitu gani na hali mchanga uliochukuliwa ni raslimali ambayo itamnufaisha mtu wa Kwale ama Kaunti ya Kwale. Kwa hayo mengi, ninaipongeza hii kamati ambayo ilitoa hii Ripoti. Pia naipongeza Serikali kwa kufikiria kwamba huu mradi utaweza kusaidia wananchi wa Kenya. Sasa tutakuwa na usafiri ambao si wa gharama ya juu kinyume na vile ilivyo katika usafiri wa ndege. Shukrani. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}