GET /api/v0.1/hansard/entries/555412/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 555412,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/555412/?format=api",
"text_counter": 169,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Gichigi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1909,
"legal_name": "Samuel Kamunye Gichigi",
"slug": "samuel-kamunye-gichigi"
},
"content": "kusikitisha sana kuwa hawa walimu ambao hata sisi wengine wao walitufundisha, tunakutana nao kule mashinani wakiumia kwa sababu ya kutolipwa pesa zao baada ya kustaafu. Serikali imechelewa sana kubadilisha mipango ya malipo ya uzeeni kwa sababu hili jambo la kuwa kila mmoja anategemea Serikali kumlipa hayo malipo ni mbaya sana. Ilikuwa ni muhimu na hata sasa nitaomba wale ambao wanahusika katika Wizari mbalimbali za Serikali waweze kutimiza mpango wa malipo ya uzeeni ambao kila mmoja anachangia; mwenye kuajiri anachangia na mwajiriwa pia anachangia. Hatutaki watu wangojee kustaafu ndio ikae kama wanaomba kutoka kwa yule ambaye amewaajiri. Hayo mabadaliko yamechelewa sana katika mipango ya Serikali. Kila wakati tunaona hata Waziri wa Fedha anaweka pesa katika Bajeti kushughulikia hilo jambo lakini baadaye huo mpango hautimizwi. Kwa hivyo, ni muhimu sana. Ni vibaya sana kwa sababu hawa waalimu walitimiza wajibu muhimu. Hii nchi haingeweza kufika mahali ilipo kama hawa walimu hawakuwafundisha wanafunzi ambao sasa ni viongozi katika hii nchi. Tatizo lililetwa na mahakama ambayo iliamuru kuwa malipo yapeanwe ambayo ni zaidi ya mishahara walimu hao walikuwa wakipata. Unakuta kuwa Ofisi ya Mkuu wa Sheria inajipata pabaya kwa sababu inaambiwa ishauri Serikali ilipe pesa ambazo kikatiba ziko na shida kidogo. Lakini kwa sababu kuna pesa ambazo zilikuwa zimetengwa na ni zaidi ya Ksh16 bilioni, ninaomba wahusika wote wawili; Tume ya Kuwaajiri Walimu na pia hao walimu ambao wamestaafu na (Technical hitch)"
}