GET /api/v0.1/hansard/entries/555414/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 555414,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/555414/?format=api",
    "text_counter": 171,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Gichigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1909,
        "legal_name": "Samuel Kamunye Gichigi",
        "slug": "samuel-kamunye-gichigi"
    },
    "content": "Ahsante sana, Mhe. Spika. Nikimalizia, nitasema kuwa katika kesi, na hata mahali ambapo pana uamuzi, kuna wakati mwingine wahusika wote wawili wanaketi chini pamoja. Ikiwa mahakama imeamuru malipo yalipwe, wanaketi pamoja kukubaliana. Kwa mfano, kama ni Kshs42 korti imesema ilipwe, basi watakaa pamoja ili kushauriana kuhusu kulipwa kwa hizo pesa hata kama ni kwa njia ya polepole. Hayo ni mambo wanastahili kuketi chini kujadili. Ninaomba maofisa katika ofisi ya Mkuu wa Sheria wasiliondokee hili jambo. Hii ni kwa sababu wanaacha Serikali pagumu sana. Mwisho, inasikitisha kuwa uamuzi wa mahakama, uamuzi wa hili Bunge na ofisi nyingine za Serikali huwa hazitiliwi mkazo. Kama Serikali yenyewe haitii uamuzi wa mahakama, wananchi wengine wanatarajiwa wafanye kitu gani? Kwa hivyo, ni muhimu sana hilo liweze kufanyika na yale mambo ambayo yanapitishwa na hili Bunge kama hili la kulipa hawa walimu liweze pia kutimizwa. Tunaunga mkono kwa nguvu. Tunaunga mkono hii Ripoti. Walimu walipwe pesa zao kwa sababu walistaafu kitambo. Ahsante Mhe. Spika."
}