GET /api/v0.1/hansard/entries/555450/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 555450,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/555450/?format=api",
"text_counter": 207,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Muzee",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2225,
"legal_name": "Daniel Kazungu Muzee",
"slug": "daniel-kazungu-muzee"
},
"content": "Ahsante sana, Mhe. Spika kwa kunipatia nafasi hii ili niongee kuhusu Mswada huu mpya ambao umeletwa katika Bunge la Taifa la Kenya. Mswada huu unahusu suala la kuwarudisha wafungwa walioko katika nchi geni ili wamalize vifungo walivyopewa katika nchi zao asilia. Shida yangu ni moja tu. Sisi Wakenya tukienda katika nchi za nje, ni vizuri kwanza tuhakikishe kuwa tunazifuata sheria za nchi ambazo tumeenda. Sharti tuheshimu na tutii sheria ili tusiingie katika shida. Kwa hivyo, ningependa kuwahimiza Wakenya wote kwamba kokote waendako sharti watilie maanani nidhamu na watii sheria za nchi ambazo wamezuru ili wasijipate kwenye shida. Vile vile wageni ambao wanakuja kwetu hapa Kenya sharti nao wahakikishe wanatii sheria zetu na wanazifuata vilivyo ili wasiingie katika matata. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}