GET /api/v0.1/hansard/entries/555453/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 555453,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/555453/?format=api",
"text_counter": 210,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Muzee",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2225,
"legal_name": "Daniel Kazungu Muzee",
"slug": "daniel-kazungu-muzee"
},
"content": "Jambo la pili ambalo nimeona, na namshukuru Mhe. Waiganjo kwa maana amelitaja, ni kwamba kuna uwezekano wa watu kutumia vipengele vya sheria hii vibaya na kuanza kuharibu mambo. Huenda mfungwa akaletwa hapa na badala ya kuendelea na kifungo chake kizungumkuti kinachezwa kisha mfungwa huyo anaachiliwa huru. Hiyo haitakuwa vizuri. Kwa hivyo, tuhakikishe kuwa tunaangazia sheria hii vilivyo ndiposa haki ifanyike. Isiwe kwamba mfungwa akishafika katika nchi yake anaachiliwa huru na hali alikuwa amefungwa kwa kutenda dhambi. Ni vizuri tuangalie suala hilo ili sheria hii isiharibiwe na wale ambao wako na mipango yao tofauti. Lakini kuna kitu ambacho ningetaka pia tuangazie zaidi. Juzi kule Africa Kusini, tuliona mfano mmoja wa mwanariadha kwa jina la Pistorius ambaye alimuua mpenzi wake na akafungwa kifungo cha miaka mitano. Ajabu ni kwamba ni juzi tu alipofungwa. Lakini saa hii tunaambiwa kwamba kuanzia mwezi wa nane, kuna uwezekano wa kuachiliwa. Unajua sheria katika nchi mbali mbali ni tofauti. Kwa hivyo, ni lazima tuhakikishe kwamba sheria za nchi zingine na sheria zetu hapa Kenya zanaambatana vilivyo ili watu wasianze kuchukua mipangilio hiyo na kujinufaisha. Kuna kipengele kinachomruhusu Mkuu wa Sheria kuamua kumuachilia mtu. Hapo ni lazima tuhakikishe kuwa haki inatendeka. Ikiwa mtu atafanya kitendo kibaya, ni lazima ahukumiwe na kuadhibiwa vilivyo."
}