GET /api/v0.1/hansard/entries/555495/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 555495,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/555495/?format=api",
"text_counter": 252,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Gathogo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2715,
"legal_name": "Esther Nyambura Gathogo",
"slug": "esther-nyambura-gathogo"
},
"content": "Wale ambao wako nje waje hapa ili waweze kuhukumiwa wakiwa karibu. Ukiwa nje haujihisi ya kwamba unataka kukaa katika nchi hiyo tena. Unataka kurudi nyumbani. Kwa hivyo, yangu ni kuunga mkono Mswada huu ili tuweze kuwasaidia watu wetu ambao wako nje. Hata wakirudi, Mhe. mwenzangu amesema ya kwamba mahali pa kulala katika magereza ya huku kwetu yako katika hali mbaya. Lazima magereza yetu yawe katika hali nzuri ili kuwafaa wale ambao wanaenda huko. Pia, magereza yanaweza kuwa katika hali nzuri lakini ile tabia wanaofanyiwa huko ni mbaya zaidi. Kwa hivyo, ni lazima tuangalie pande zote ili wakiingia huko, wakae kwa njia ambayo inafaa kwa Mkenya yeyote. Asante Mhe.Naibu Spika wa Muda. Naunga mkono."
}