GET /api/v0.1/hansard/entries/555881/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 555881,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/555881/?format=api",
"text_counter": 283,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Lay",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1022,
"legal_name": "Joyce Wanjalah Lay",
"slug": "joyce-wanjalah-lay"
},
"content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa ya kuchangia Hoja hii ambayo Mhe. Injendi ameleta. Kwa kweli, nataka pia kumpongeza kwa sababu imekuja kwa wakati unaofaa. Nakumbuka mwezi uliopita nilikuwa na mkutano kule Taita na viongozi wa makanisa. Hili lilikuwa ni swala tetesi. Walizungumza na kutuambia kuwa hapa Bungeni, tulete Hoja hii ili tuhakikishe kuwa ofisi za kusajili ndoa zimeletwa karibu na kaunti. Mhe. Injendi alitangulia kwa kuongea kuhusu mambo ya fedha zile ambazo watu wanaitishwa wakati wanapoenda kusajili harusi au ndoa. Kwa kweli, fedha hizi zinazoitishwa ni nyingi mno. Unapata kuwa inakuwa ni vigumu na vijana ambao wanatarajia kuoa wanaogopa kwa sababu ya fedha ambazo wanaitishwa. Vile vile, unapata vijana wetu wengi hawana kazi, gharama ya maisha imepanda na kila kitu ni bei ghali. Tukisema kwamba pia katika ndoa tuweke bei ghali, itakuwa vigumu sana kwa vijana wetu kuweza kuingia katika ndoa halali. Alizungumza kuhusu cheti cha ndoa. Wakati huo mwingine kilikuwa Kshs200, lakini saa hii kimefika Kshs500. Kuhalalisha ndoa ilikuwa Kshs1,000, lakini saa hii ni Kshs2,000. Na vile vile kuna swala la kumpa cheti yule ambaye anafunga ndoa. Wakati uliopita ilikuwa hawaitishwi chochote, lakini sasa hivi ni Kshs1,000. Kwa kweli, unapata kuwa ni gharama na haitakuwa rahisi kwa sisi kushangilia ndoa nyingi ambazo zitakuwa zinafungwa kihalali. Hoja hii inazungumzia kuhakikisha kwamba ofisi ambazo zinasajili ndoa ziletwe karibu na mahali ambapo wananchi wanaishi, ikiwezekana katika kaunti zote ama sehemu tunazoita kwa Kiingereza “ sub-county” . Sasa hivi nchini Kenya, ziko afisi 12 pekee za kuandikisha ndoa, na ziko katika miji mikubwa mikubwa. Kama kwetu Taita Taveta, inabidi mtu aende Mombasa ili asajili notisi kwamba anataka kupewa ruhusa ya kumoa mpenzi wake. Kama vile Mhe. ametangulia kusema, miezi mitatu inayohitajika ni mingi. Anasema kwamba kuna wasiwasi katika miezi hiyo mitatu kuwa yule mchumba anaweza kuchukuliwa na mtu mwingine; ukapata kwamba unakosa mchumba wako wa kufunga ndoa. Kusafiri kutoka mahali ambapo wananchi wanaishi hadi kituo kingine ambacho ni cha msajili wa Ndoa ni mbali sana na wananchi. Ni jambo la muhimu kuhakikisha kwamba vituo vya usajili vimeletwa karibu na kila jiji."
}