GET /api/v0.1/hansard/entries/555914/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 555914,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/555914/?format=api",
    "text_counter": 316,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Aburi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2901,
        "legal_name": "Lawrence Mpuru Aburi",
        "slug": "lawrence-mpuru-aburi"
    },
    "content": ", katika ukurasa wa tatu, utapata “mizigo” ya mwanaume. Unaelewa “mizigo” ya mwanaume. Hatuwezi kuitaja lakini kila mtu anaielewa. Wanawake wa Nyeri wakifanya harusi, baada ya kupewa vyeti, wanangoja wakati wanaume wamelewa pombe ama wamelala kisha wanakuja na kisu na kung’oa kila kitu. Sisi wanaume tumechokeshwa na hawa akina mama. Ndio maana nasema hata ni shida kuunganishwa katika ndoa. Mimi natetea wanaume kwa sababu wanawake wamekuwa shida kwetu. Lazima tuende polepole na tuelewane na akina mama kwamba, “Mimi nimekuoa uwe bibi yangu. Nimeunganishwa na wewe na kuwekwa pete na nitakaa pamoja na wewe.” Hakuna maana ya mama kutoheshimu bwana yake. Lazima uniheshimu na mimi nikuheshimu ndio tuweze kukaa pamoja. Hata tukienda kuunganishwa,wakati mwingine kuna wale wakora. Unaunganishwa nao lakini yeye analenga ile mali ambayo unayo kama magari na nyumba. Akiingia kwa nyumba, anakuwa simba; huwezi hata kuongea wala kuinuka. Hilo ni jambo baya sana. Sisi wanaume tunasema kwamba kile kitendo kilitendeka Nyeri kwa Wakikuyu si kizuri. Ni kitendo kibaya sana kung’oa mwanaume “mizigo” yake. Wewe mama unang’oa mali ya mwanaume na hiyo mali ndio inakufurahisha ! Ni vibaya sana. Mimi ninaunga mkono Hoja hii lakini hilo jambo la kung’oa vitu vya wanaume sitaki."
}