HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 556420,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/556420/?format=api",
"text_counter": 171,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "kuchukua hisa za yale makampuni mengine ya mafuta yalikuwa kwanza kuboresha kiwanda hicho ili kiwe kinasafisha mafuta ndio tupate kiwango ambacho kinahitajika cha mafuta na cha kuridhisha. Mhe. Naibu Spika wa Muda, utaelezwa na hii Ripoti ukiisoma kwa undani kuwa waliohusika na ubinafsishaji wa kiwanda hicho, waliweka mikakati ya vile hiyo kampuni itaingia, ianze kazi, ichukue hisa na ihakikishe kuwa kiwanda kimeboreshwa kabisa na shida ya mafuta imeisha. Ilikuwa pia ihakikishe kuwa usafishaji ulikuwa mzuri, Serikali itapata faida na wafanyikazi wa kiwanda cha mafuta nao pia watakuwa wamepata nafasi. Suala likawa US$15 milioni ndizo hela kampuni hiyo ingelipa Serikali. Baadaye, kwa sababu ambazo hazikueleweka, na mpaka sasa hakuna mtu ambaye ameeleza, ikawa hawatalipa US$15 milioni bali watalipa US$2 milioni. Hata hundi hiyo ya US$2 milioni ilipotolewa, ilizungushwa kati ya Wizara ya Fedha na kiwanda hicho cha mafuta kwa muda wa miezi sita, bila ya kujua ni nani aliyepaswa kuipokea hundi hiyo mpaka muda wake wa kulipwa ukaisha. Kwa hivyo, inabainika wazi kwamba kampuni hiyo ya Mauritius haikulipa chochote kukibinafsisha kiwanda hicho. Mhe. Naibu Spika wa Muda, katika mikataba ambayo waliweka, walikubaliana kwamba muda ukifika na watu hao washindwe kukiboresha kiwanda hicho, watalipwa US$5 milioni na Serikali. Swali ambalo unapaswa kujiuliza ni: Kwa nini Serikali ilipe US$5 milioni kwa mtu ambaye alikuja kununua asilimia 50 za hisa za kiwanda ambacho kinafanya kazi? Kwa nini mtu huyo, ambaye aliahidi kukiboresha kiwanda hicho, alipwe fedha hizo na kuondoka anaposhindwa kukiboresha kiwanda hicho? Hii inamaanisha kwamba nchi hii imepoteza hisa zake, US$15 milioni, na ikapoteza muda tukitarajia kuwa kiwanda kitaboreshwa. Tunavyozungumza, wafanyikazi hawana chochote. Kiwanda kimefungwa; hakifanyi kazi. Wafanyikazi wamepoteza ajira yao. Wakazi wa Pwani tumekuwa tukijivunia kwamba tulikuwa na mtambo wa kusafisha mafuta kule Changamwe. Mtambo huo haupo tena. Sasa imebaki fedheha. Kimekuwa kitu cha kuangalia tu. Zamani kulikuwa na mtambo wa mafuta. Sasa kilichobaki ni vyuma vinavyoshika kutu. Ardhi yenyewe inaelekea kuuzwa; ina utata. Lililobaki ni kujiuliza, je, wale waliohusika, walikuwa na madhumuni gani? Nia yao ilikuwa ni nini? Je, nia yao ilikuwa ni kukiboresha kiwanda hicho ama nia yao ilikuwa, kwanza, kwenda Muritius na kuanzisha kampuni ya kununua hisa za kiwanda hicho? Kwa nini Mauritius? Kwa sababu Mauritius ni nchi ambayo inaficha siri za wahusika wa makampuni. Pili, Serikali ya Mauritius haitozi kodi. Tatu, wafisadi wakuu ulimwenguni huenda kujificha huko. Wahusika ni wakuu serikalini wanaoshikilia nyadhifa mbali mbali, haswa wakuu wa kitengo cha uboreshaji na ubinafsishaji wa mashirika ya umma nchini, na wakuu katika kiwanda hicho, ambao baadhi yao wao wameondoka baada ya kukipora kiwanda hicho. Baada ya kufanya hizo mbinu zote, baadhi yao wakaenda kuchukua nyadhifa za kisiasa. Je, tutaendelea na mambo kama haya nchini kwa muda gani? Mhe. Naibu Spika wa Muda, Wizara ya Kawi ilikuwa imetuahidi kuwa kiwanda hicho kikiboreshwa, bei ya mafuta ingepungua na tungekuwa na bidhaa za mafuta za kutosha. Kama unakumbuka, kuna wakati watu walianza kupiga foleni kununua mafuta kwa sababu ya uhaba wa mafuta. Washikadau katika sekta ya mafuta nchini walikuwa wakibishana na Serikali, wakiulizana ni nani aliyepaswa kuleta mafuta yaliyosafishwa, na ni nani aliyepaswa kuleta mafuta ambayo hayakuwa yamesafishwa ili yasafishwe kwenye kiwanda hicho. Kukawa na shida ya mafuta. Wamiliki wa Kampuni ya Essar ya Mauritius walipokuja, walisema kwamba The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}