GET /api/v0.1/hansard/entries/556421/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 556421,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/556421/?format=api",
    "text_counter": 172,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "shida ile ingeisha kwa sababu wangekiboresha kiwanda hicho ili kiweze kutoa mafuta masafi na nchi itafaidika. Tunashangaa ni masaibu gani ambayo yameikumba nchi hii? Jambo la kushangaza ni kwamba watu wote wanaokuja nchini kushiriki kwenye mpango wa ubinafsishaji wa viwanda na makampuni yetu, nia yao ni kupora mali ya nchi hii. Kwa mfano, ni nani ambaye hajui kwamba Telkom Kenya lilikuwa shirika kubwa ambalo halikuwa linatingisika? Lakini limeuzwa na ukiangalia jinsi lilivyouzwa, utaona kwamba hisa zimeporwa na hivi sasa wafanyikazi wa shirika hilo hawana ajira. Shirika limechukua mkondo huo. Hivi sasa, wameshikana na shirika la Wareno, ambao wanasema wanaliboresha shirika na ndege nchini. Wamenunua ndege, lakini madhumuni yao ni nini?"
}