GET /api/v0.1/hansard/entries/557093/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 557093,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/557093/?format=api",
    "text_counter": 111,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Ahsante, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Naomba nami nichangie Hoja hii kuhusu gharama za ndoa na vile ndoa zimekuwa haziwezi kufanyika hivi sasa kwa sababu ya matatizo ambayo yameletwa hasa na Serikali. Tulipopitisha Mswada wa Ndoa wakati mwingine, hatukutarajia kuwa baadaye Serikali itageuka iseme kuwa itaweka sheria ya kusema kuwa yule ambaye anataka kufunga ndoa lazima asafiri hadi makao makuu ambayo yamepangwa na Serikali. Nikitoa mfano, watu wangu wa Taita watoke Taita waende Mombasa ama waje Nairobi ndio waweze kupata cheti cha ndoa."
}