GET /api/v0.1/hansard/entries/557094/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 557094,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/557094/?format=api",
"text_counter": 112,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Utakubaliana nami kuwa cheti cha ndoa ni muhimu na kila mtu anakihitaji ili kuthibitisha kuwa amefunga ndoa na mtu na kuwa wale watoto ambao Mungu amewajalia mkapata wametokana na ile ndoa mliofunga. Tatu, mmoja wenu akiwa hayupo na ameaga ndunia, mali mtaigawanya namna gani ama ni nani ataachiwa mali? Mkiwa mnamiliki mali, nani ataweza kumiliki hiyo mali? Lakini hivi sasa, imekuwa ni kero kubwa kwa mtu yeyote anayetaka kuoa mwenzake ama kuolewa na mwenzake. Inambidi, licha ya kutoa mahari, agharamie usafiri kwenda kutafuta cheti na asajiliwe. Badaye, ndio arudi tena kanisani kuja kufunga ndoa. Swali tunalouliza ni: Kwa nini tumeweka sheria kama hizi ambazo zinafanya watu washindwe kufunga ndoa ama kuoana? Je, nia yetu tulipokuwa tunapitisha Sheria ya kuoana ilikuwa kuleta gharama ambazo binadamu ama wananchi hawawezi kuzigharamia na baadaye kuanzisha mipango ya watu tu kuungana? Binti atoke nyumbani kwao aende akae na mwanaume. Wazungu wanasema The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}