GET /api/v0.1/hansard/entries/557097/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 557097,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/557097/?format=api",
"text_counter": 115,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Ndugu zetu waislamu wana bahati. Hawakuhusishwa na sheria hii kwa sababu makadhi kokote walipo wanaweza kufungisha ndoa zao. Lakini sisi wakristo tuna shida kubwa sana kwa vile watu lazima wasafiri ndio waende kupata vyeti. Halafu ile ilani ambayo inahitajika ni kubwa. Unatakiwa kutoa ilani siku 21. Katika wakati huo, hauwezi kupanga kitu chochote kwa sababu haujui ikiwa ilani italeta kero na mtu mwingine ataenda asimamishe hiyo ndoa. Kwa hivyo, tunaomba kuwa gharama za ndoa zirudi chini. Tuhakikishe kuwa ofisi zimetengwa katika kila sehemu ya kaunti. Watu waweze kufungishwa ndoa na wale ambao watasajiliwa kuweza kupeana vyeti wawe ni watu wa kuaminika, wamehitimu na wanaheshimika."
}