GET /api/v0.1/hansard/entries/557111/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 557111,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/557111/?format=api",
    "text_counter": 129,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Leshoomo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 379,
        "legal_name": "Maison Leshoomo",
        "slug": "maison-leshoomo"
    },
    "content": "Katika jamii hiyo, ukifunga ndoa bila ya ng’ombe ndume kuchinjwa asubuhi, wewe bado hujaolewa! Ukiwambia Wasamburu eti uko na cheti cha ndoa kutoka kortini ama kwa DC, hawatakitambua cheti hicho. Sheria za ndoa zitakuwa muhimu sana ikiwa zitashikanishwa na sheria za ndoa za kitamaduni. Hiyo ni kwa sababu katika jamii, kuna watu ambao wanaamini kwamba ndoa za kitamaduni ni bora kuliko ndoa za Serikali. Kwa hivyo, inafaa ndoa zote zishikanishwe, na kila mtu ajue kwamba aina zote za ndoa zimeshikanishwa. Hatufai kutupilia mbali ndoa za kitamaduni na kufuata ndoa aina nyingine. Kulingana na sheria hii, tunafaa kujua watu wataenda wapi kuoana. Watu wanaenda kuoana kwenye chumba, halafu wanabeba cheti na kusema wameoana, ilhali familia zao hazina habari kuhusu ndoa hiyo."
}