GET /api/v0.1/hansard/entries/557126/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 557126,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/557126/?format=api",
"text_counter": 144,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Amolo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 631,
"legal_name": "Rachel Ameso Amolo",
"slug": "rachel-ameso-amolo"
},
"content": "Ahsante sana, Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuchangia Hoja hii kuhusu ndoa. Ndoa ni jambo takatifu kama sisi sote tunavyofahamu. Ndoa hutoka kwa Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye hupeana vitu vizuri kwa viumbe vyake. Katika Hoja hii, tunaangalia gharama ya ndoa na vile tunaweza kupanga mambo haya ili yaweze kuwa sambamba kwa watu wetu kule mashinani. Kwa mfano, kule magharibi mwa Kenya ambapo tuna majimbo matano na watu karibu milioni sita, tunategemea msajili mmoja ambaye yupo pale Kakamega. Kwa hivyo, inakuwa ni gharama sana kwa mtu kutoka kule Busia, Vihiga, Trans-Nzoia na Bungoma kwenda Kakamega kwa sababu ya ndoa tu. Inawatia vijana wetu uvivu wa kutafuta nauli ili wafike kule Kakamega kumtafuta msajili huyo. Ingekuwa ni jambo nzuri kama tungekuwa na hao wasajili katika kila jimbo ili vijana wetu katika mashinani, ambao kazi wanazopata ni vibarua vya hapa na pale, waweze kuchangia wafike pale Kakamega kuangalia namna watapata kuoa bibi watakaoishi nao. Lazima tuwape vijana wetu nguvu ili waoe katika ile njia itakayowafaidi siku zao za usoni. Tunapowatia uvivu bila kuwapatia ile nguvu, ule muda ambao wamepewa kungoja mpaka vile vyeti vipitishwe huwa mrefu sana. Inawafanya wale vijana wakose hamu ya kuoa kwa sababu wanaona kuwa itawachukua muda mrefu. Mbali na hayo, itachukua senti zao nyingi. Afadhali atafute msichana ambaye anaweza kuishi naye. Yule atakayemkubali bila gharama yoyote. Kama vile kuchukua kipande ni bure na akina mama wanapojifungua watoto wanapata kile cheti bure, ningeomba Serikali ifanye hivyo hivyo ili unapooa, pasiwe na yale malipo. Wewe mwenyewe umempenda yule msichana na yeye pia amekupenda. Sioni kwa nini kuwe na gharama kubwa sana ya kuwafanya watu hao wawili wasiishi pamoja na wajenge nchi yetu ya Kenya. Sheria itabaki vile vile. Tunaangalia gharama tu na vile tunaweza kuwa na hao wasajili karibu na watu wetu ili mambo yetu ya ndoa yawe sambamba. Tungeomba irudishwe vile ilivyokuwa pale mbeleni ili unapoingia kanisani na kufunga ndoa, upewe kile cheti mara moja. Usiwe tena na kazi ya kuenda kukitafuta hapa na pale. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}