GET /api/v0.1/hansard/entries/557744/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 557744,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/557744/?format=api",
"text_counter": 23,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Wekesa",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2742,
"legal_name": "David Wafula Wekesa",
"slug": "david-wafula-wekesa"
},
"content": "Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii ili nami niunge mkono malalamishi ambayo yamewasilishwa na Mhe. Chris Wamalwa Wakhungu. Sisi sote tunajua kwamba Serikali na watu wetu wanategemea machifu na manaibu wao kwa kazi nyingi, kama vile kupata vitambulisho na mambo mengine. Hao ndio wanawatambua wakazi wa sehemu zao kwa sababu wanakaa nao. Maandamano ambayo yalikuwa kule Mabonde yalisababisha hasara kubwa. Mali nyingi iliharibiwa. Kwa hivyo, ni muhimu machifu wakiajiliwa ama kupandishwa vyeo, wawe wanatoka sehemu ambazo wamezaliwa. Kwa hayo machache, naunga mkono."
}