GET /api/v0.1/hansard/entries/560310/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 560310,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/560310/?format=api",
    "text_counter": 135,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Mheshimiwa Spika, ninashukuru kwa nafasi hii. Ninasimama kuyaunga mkono majina haya ili yaweze kupitishwa mara moja na kufanya kazi inayohitajika. Ninaungana na wenzangu nikisema kwamba ni aibu kubwa sana kuona kwamba sisi Maseneta tuliochaguliwa na kura nyingi kuliko wao ukizingatia kura ambayo kila Seneta alipata, kuona kwamba jambo lolote likipitishwa hapa, likifika kwao wanalifanyia mzaha. Bw. Spika, ninakushukuru sana kwa taarifa uliyotoa hapa leo na kwa msimamo wako ambao umesimama nao kutoka mwanzo kuhusiana na Bunge la Seneti na Bunge la Kitaifa. Sisi tumechaguliwa kuilinda Katiba. Rais pia yuko pale kulinda Katiba. Lazima tuongozwe na Katiba na sheria tunazopitisha hapa. Kama kila mtu atakuwa anafanya anayoyafikiria bila kuzingatia Katiba, taifa hili litaelekea katika njia panda na mwisho litapotea. Hakutakuwa na mtu hata mmoja anayestahili kutii sheria. Jambo lililofanywa na Wabunge wa Bunge la Taifa ni jambo la aibu sana. Mheshimiwa Spika, nakuhimiza usimame na msimamo huo, usitingizwe na mtu na usishtuliwe na jambo lolote kwa sababu unasimama kulingana na Katiba. Utadhulumiwa na kuitwa majina. Seneti itadunishwa na kuitwa “Nyumba ya wazee” waliostaafu. Wewe ni mmoja wao, lakini usitingizike. Simama imara ili tuweze kuliongoza taifa hili kwa sheria taratibu na vile mambo yamepangwa. Kwa hayo machache, Bw, Spika, ninaunga mkono."
}