GET /api/v0.1/hansard/entries/560327/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 560327,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/560327/?format=api",
"text_counter": 152,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Machage",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 179,
"legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
"slug": "wilfred-machage"
},
"content": "Bw. Spika, siku ya leo itaangazwa katika historia ya Kenya kama siku nzuri; siku ambayo wateule waliteuliwa kuangaza mawazo yao kwa sheria za nchi, hii ambazo huenda awali hazikuzingatiwa kwa hekima iliyostahili. Wakati wa kupata Katiba mpya kulikuwa na mawazo mengi. Kundi moja lilisema kwamba Katiba haifai; irekebishwe kabla kupitishwa. Kundi linguine likasema Katiba ipitishwe ndipo irekebishwe. Wale wa upili wakashinda uchaguzi. Bw. Naibu Spika, wakati umefika ambapo Katiba hii ambayo makundi haya mawili yaliona na kukubaliana kwamba kuna vipengele ambavyo havikufaa na vinahitaji kurekebishwa, basi irekebishwe. Kati ya vipengele ambavyo havikufaa kabisa ni nguvu za Seneti. Ulimwengu mzima, Bunge la Seneti limekuwa la heshima na nguvu kiwango fulani ambazo zinatumika hasa kuleta na kuieweka nchi kuwa na amani, ushirikiano na uwiano. Kwa sababu ya siasa za wengine, nguvu hizii ziliondolewa kabisa kwa Seneti hii. Katika kikao cha Bomas cha kwanza na cha pili, nguvu za Seneti zilizingatiwa na zilikuwa nzuri. Kikao cha Kilifi kikaja na kikao ambacho kiliharibu hasa ni kile cha Naivasha. Kwa sababu ambazo hazijaeleweka hadi wakati huu, nguvu za Seneti zilipunguzwa kabisa hadi kiwango cha Seneti tuliyonayo wakati huu, wakati mwingine hata “Bunge la taifa” husahau na kupuuza kabisa kuwepo kwa Seneti katika umoja wa Bunge la Taifa. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}