GET /api/v0.1/hansard/entries/560330/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 560330,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/560330/?format=api",
"text_counter": 155,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Leo kabla Hoja hii, tumeona makosa kama hayo. Wakati mwingine ninafikiri hata Rais wa nchi husahau kwamba kuna Seneti au hupotoshwa mawazo ili asiangaze mawazo yake na hekima atafute mawazo ya Seneti kwa mambo mengine ambayo ni muhimu kwa nchi hii. Kundi hili la watu tisa limeteuliwa litembee, likae na lifanye chochote kinachowezekana kukusanya maoni ya wanasiasa, wananchi, Wabunge na hali kadhalika.Linapaswa kuangalia ni vipengele gani vya Katiba ambavyo vinahitaji kurekebishwa ili Seneti iwe Bunge la heshima na linalostahili sifa zake. Watu hawa wamechaguliwa kutoka kwa milengo yote miwili ya siasa katika Bunge hili kwa uangalifu na uadilifu. Bw. Naibu Spika, wanawake kwa wanaume waliochaguliwa wamepewa jukumu kubwa. Ningetaka kwamba mawazo yao yasije yakafungwa na siasa za kufikiria kwamba sasa ni siasa za “Okoa Kenya”,“Pesa Mashinani” au hili na lile. Hawa wote labda wana mawazo mazuri ya kukusanya kutoka kwao.“Okoa Kenya” na “Pesa Mashinani” wasikizwe. Sijui sisi tutajiita nini lakini kama itabidi tuunganishe haya majina na tulete jina lingine la tatu, ni sawa. Jina halijalishi kabisa. Hekima ndio muhimu. Mambo ambayo wataibuka nayo kwa minajili ya kurekebisha vipengele vya sheria vinavyohusu Bunge hili yafanywe kwa uangalifu na kwa undani, wachimbe na kuchimbua yale yote ambayo tumesema tangu mwanzo wa Bunge hili hadi sasa. Tulianza vizuri. Nakumbuka katika miezi sita ya kwanza kulikuwa na fikira za kuwa na kikundi kama hiki cha kurekebisha sheria zilizopo ili mradi kuwe na Serikali nzuri hasa kipengele cha Bunge la Seneti. Haya mawazo yalipotoshwa kwa sababu ya siasa duni. Wenzetu ambao walipotosha mawazo ya kwanza bado wapo na bado watajitokeza. Kutakuwa na wimbi la kupotosha mawazo ya kamati hii ambayo tumeteuwa leo ili wasahau lengo la jukumu lao. Bw. Naibu Spika, ombi langu ni kwamba ninyi muwe wacheshi na wenye fikira za hekima na msipotoshwe kamwe na mawazo ya wale wasiolenga wema kwa Bunge hili. Tunataka Kamati hii iangaze mawazo yake kwa sheria na shida zote tulizopitia na kustahimili katika Bunge hili. Pia, tunataka waanze mawazo yao kwa ujenzi wa Taifa la Kenya ili liwe la heri na kuangaza mawazo yao kwa utukufu wa Bunge hili katika siku za usoni. Tunataka mawazo yao yawe ya ujenzi wa taifa la Kenya na utu uzima. Hilo ndilo ombi langu kwa kundi hili la wateule ambao leo twapitisha katika Bunge hili hivi leo. Hili si jukumu ndogo; jukumu lao ni kubwa. Huenda hata wasipate nafasi ya kukaa kwenye vikao vingi vya Seneti, lakini itabidi wastahimili yote watakayoyapitia ilimradi waje na stakabadhi za sheria ambazo wao watakuwa wameangazia ili nasi tuyafikirie. Kundi hili la Maseneta lina wanasheria karibu watatu hivi. Wengine wana masomo tofauti; kuna wanahesabu, waalimu na kadhalika. Kwa hivyo, hili ni kundi The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}