GET /api/v0.1/hansard/entries/560332/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 560332,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/560332/?format=api",
"text_counter": 157,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "ambalo limeteuliwa kwa kuangalifu. Ni kundi ambalo litakuwa na fikra ambazo zimejaa kwa kuangaza mawazo yao kwa sheria ambazo zinastihili kurekebishwa. Bw. Naibu Spika, tunajua kwamba Bunge la Kitaifa linangoja kwamba baada ya kupitisha ama kuangaza mawazo yetu kwa sheria fulani, wao wazivunje na kuziangusha. Lakini ningependa kuwaambia kwamba nguvu zetu ni nguvu za wananchi mashinani na sheria ambazo zitapitishwa au ambazo zitaangaziwa mawazo yetu, zitapelekwa mashinani kwa wananchi wenyewe kuamua kama zinatosha ama hazitoshi. Tunataka waelewe kwamba sheria hizo zitapitishwa na wananchi na watabaki wakisaga meno kwa sababu wananchi pia wanaona yale yanayotendeka na wamesoma. Wananchi wanajua ni Bunge gani linafaa kupewa nguvu za kutosha kwa uongozi wa Taifa la Kenya. Ombi langu kwa wananchi ni kwamba waoembee kamati hii dua njema na iwapo watahitajika kuja kupendekeza mawazo yao, waje kwa dhati na hima ili wayaangaze mawazo hayo kwa vipengele ambavyo wanafikiria vinahitaji marekebisho. Bw. Naibu Spika, naomba kuunga Hoja hii."
}