GET /api/v0.1/hansard/entries/560348/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 560348,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/560348/?format=api",
"text_counter": 173,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "jukumu lake. Lakini lazima bunge hizi ziungane mikono katika kazi zao. Tukiangalia Bunge la Taifa na Seneti, kumekuwa na mgongano kila mara. Kwa mfano, kuna Miswada ambayo ililetwa kutoka Bunge la Taifa lakini ikija hapa, pengine Seneti inakataa kuipitisha. Bw. Naibu Spika, tumejaribu njia nyingi bila mafanikio. Tulipoanza, tulienda kortini kuuliza ufafanuzi wao vile tunavyotakikana kufanya na walifanya hivyo. Baadaye, tulikuwa na mkutano mkubwa ambao ulifanyika mwaka wa uliopita ambapo tulikuwa na wawakilishi tofauti tofauti kutoka korti mbalimbali. Tuliwauliza jinsi ya kuendeleza kazi ya Seneti na tukakubaliana juu ya mambo fulani. Hata hivyo, imekuwa kama kawaida kwamba wakati wowote jambo lolote likija hapa, hasa Mswada, tunagombana. Basi wakati ni huu. Kama wakati si sasa, basi ni sasa hivi kusimama kama Seneti. Maseneta wengine wamesema kwamba itabidi tusimame kwa umoja. Waliochaguliwa kuunda kamati ni Maseneta ambao wamepewa kazi ngumu. Kazi hiyo ni muhimu. Hii ni kwa sababu itabidi waangalie vipengele tofauti tofauti katika Katiba. Wanafaa kuangalia vile ambavyo vinaweza kubadilisha na kuzungumza na wananchi kwa sababu lazima kuwe na Bunge la kusema neno la mwisho. Kwa mfano, tukiangalia nchi kama Rwanda, Uingereza au “Amerikana”, tunaona kwamba wameweza kuweka mikakati vile ambavyo sheria ambayo itatoka ‘”Nyumba” moja hadi nyingine. Haswa katika sheria hizi kuna uwazi, kwamba kuna “Bunge la Taifa” na “Bunge la Seneti.” Mara nyingi kama kuna Mswada ambao umetokea, mwisho ile “Nyumba Kuu” ndio inatakikana ielekeze na iwe na uamuz wa mwisho kuhusu Mswada ule. Tunajua kwamba Katiba haisemi kuwa kuna “Nyumba Kuu” na “Nyumba ya Chini.” Kwa hivyo, tunafaa kuangalia sheria na Katiba na kuamua ni vipi ambavyo tutafanye kazi kwa pamoja. Tuangalie vipengele tofauti ambavyo vinahitaji kurekebishwa. Bwana “Mzungumzishi”, tumefika mahali ambapo tunafikiria kwamba vipengele hivi visipoangaliwa na kurekebishwa, itakuwa vigumu sana kwa Seneti kufanya kazi yake. Juzi tuliwaona Sen. Mutula Kilonzo Jnr. na Sen. Murkomen wakihojiwa katika stesheni moja ya runinga nchini. Ile habari kutoka kwa wananchi ilikuwa inaonyesha mapendekezo yao kuhusu Seneti. Bila Seneti hakuna ugatuzi. Hilo ni jambo ambalo ni lazima tulielewe. Kama tunataka ugatuzi ni lazima tuwe na Seneti. Kama hatutakuwa na Seneti ambayo imepewa nguvu ambayo inahitaji ili itekeleze wajibu wake wa kutetea kaunti na serikali zao, itakuwa vigumu sana. Ni vizuri kwamba Kamati hii imechaguliwa. Inafaa iangalie mambo yote ikiwemo historia ambayo tumekuwa nayo na pia sheria ambazo tumeweza kuzipendekeza. Iangalie hata yale mambo ambayo Seneti imependekeza. Kwa mfano, tulikuwa tumesema kwamba tutakuwa na vikao katika kaunti. Vikao hivi vitawaunganisha viongozi wote. Hata sasa nimezungumza na viongozi tofauti tofauti ambao wamesema kwamba sisi kama Seneti tulifanya jambo la maana na tunaweza kuwaweka pamoja viongozi wote ili wazungumzie mambo kadhaa. Hata hivyo, vikao katika kaunti havikufanyika na kwa sababu hiyo, watu wamedhoofika. Pia, kuna sheria ambazo tumeweka lakini hatujaweza kuziendeleza mpaka ziwanufaishe haswa wale ambao wanangojea ugatuzi. Tuziangalie zimekwama wapi na The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}