GET /api/v0.1/hansard/entries/560350/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 560350,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/560350/?format=api",
"text_counter": 175,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "tujue jinsi ya kuzikwamua. Tukumbuke pia kwamba hili ni Bunge ambalo sasa lina “Nyumba” mbili. Tuangalie kwa nini Seneti ya kwanza haikuweza kuendelea na kazi yake. Tuangalie ikiwa nguvu za Seneti hiyo ndio chanzo chake kuvunjwa kwa haraka. Hatutaki Seneti ya pili ivunjwe kwa haraka vile. Nina imani na nimewasikia wananchi wengi wakisema kwamba tunahitaji Seneti. Wakati ni huu. Ninawapongeza wanakamati ambao wameteuliwa kwa Kamati hii ya muda. Niwaombea wafanye kazi njema ambayo itaimarisha Seneti na miaka nyingi itakayokuja tutasema kwamba kweli Kamati ile ilifanya vyema. Asante, Bwana “Mzungumzishi”."
}