GET /api/v0.1/hansard/entries/561068/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 561068,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/561068/?format=api",
    "text_counter": 74,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Nakushukuru, Mhe. Naibu Spika, kwa nafasi hii ambayo umenipatia. Kitu cha kwanza ni kuwapongeza wenzangu katika Kamati hii ya kuangalia Makadirio ya Fedha kwa kazi ambayo wamefanya ya kuridhisha, ijapokuwa mara ya kwanza tulikuwa tumeshikwa na ghadhabu kwa yale waliofanya. Lakini nashukuru Mungu. Wakiongozwa na ndugu yangu Mheshimiwa Mutava Musyimi, wamefanya marekebisho ambayo yamekubalika na hivi sasa, tuko katika kiwango cha kuangalia ugavi wa fedha za Serikali. Ugavi au ugawaji huu katika wakati huu umechukuwa mwelekeo mpya kwani fedha hizi zimegawanywa kulingana na mipango ya Serikali. Ile miradi ambayo imekubalika ndio itakayofanywa, ndipo hapo fedha zimeelekezwa. Ni jukumu la Wabunge kuhakikisha kuwa wanafuatilia kwa uangalifu waone kuwa fedha hizi zinatumika kwa kazi ama mipango ile ambayo imewasilishwa Bungeni. La sivyo, itakuwa ni jambo la fedheha sisi kukaa hapa, The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}