GET /api/v0.1/hansard/entries/561071/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 561071,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/561071/?format=api",
    "text_counter": 77,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": ". Lile ambalo naona bado lina kero ni fedha ambazo zimewekwa katika kitengo cha elimu. Hapo awali, tulikuwa tumeweka Ksh11,000 kwa kila mwanafunzi kwa mwaka. Sasa zimeongezwa zimefika Ksh13,000 kwa mwaka kwa kila mwanafunzi. Lakini tukiangalia Ksh13,000 kwa kila mwanafunzi, haziwezi kufadhili mwanafunzi kusoma kwa mwaka mzima. Ndio maana katikati, unaona kila wakati wanafunzi wanaambiwa warudi nyumbani. Tunatarajia wakati utafika ambapo tutasema kuwa kama elimu ya sekondari inafadhiliwa kikamilifu na Serikali, basi iwe kweli inafadhiliwa kikamilifu na Serikali. Fedha zitengwe za kutosha. Wanafunzi wakilipiwa karo, basi wajue wanaenda muhula wa kwanza mpaka wamalize muhula wa mwisho bila kuambiwa na walimu warudi nyumbani. Tukiangalia ni kuwa ile hazina ambayo ilikuwa inatolewa kwa wanafunzi wa sekondari katika Makadirio haya imeondolewa. Hiyo najua itakuwa changamoto. Kwa hivyo, itabidi kila mzazi aangalie atafanya nini. Bila shaka, itatulazimu tuangalie vile Hazina ya Ustawi wa Maeneo Bunge (CDF) itakavyotumika kufadhili wanafunzi hao. Kuna fedha ambazo zimewekwa za kuajiri walimu - Ksh4 bilioni. Tukiangalia hali ya nchi vile ilivyo, walimu wanaohitajika ni wengi na sioni kama fedha hizo zitatosha. Ni ombi langu tuanze kufikiria ni wapi tena tutatoa pesa za kufadhili uajiri wa walimu. La sivyo, kuna sehemu za nchi ambazo walimu hawatoshi na imebidi wazazi wenyewe wajifunge kibwebwe ili waangalie kuwa walimu wanaajiriwa. Wazazi wenyewe ndio wanaowalipa. Je, pale ambapo wazazi hawana uwezo wa kuajiri hao walimu, itakuwa namna gani? Nikiangalia, kuna Hazina Sawazishi kwa Kiingereza inaitwa Equalisation Fund. Mpaka sasa, hizo fedha bado ziko katika Benki Kuu ya Kenya na hazijawahi kutumika tangu tuanze Katiba mpya. Sheria zake bado hazijaletwa hapa Bungeni na najua zina utata. Hazina hiyo ilikuwa imewekwa katika Katiba yetu ili tuangalie sehemu ambazo hazijaendelea au kustawi ili zipewe fedha hizo ili zipate kustawi kama maeneo mengine. Namwomba Mwenyekiti wa Kamati ya Makadirio aangalie kikamilifu hazina hiyo - namtafsiria kuwa inaitwa Equalisation Fund kwa Kiingereza, yaani Hazina Sawazishi. Kwa nini hizo fedha mpaka sasa bado ziko katika Benki Kuu ya Kenya na hazijatumika? Tunaambiwa kuwa hawataki. Ni akina nani ambao hawataki? Kwa mujibu wa Katiba, maeneo ambayo hayajastawi kufikia viwango vya maeneo ambayo yamestawi yanastahili kupewa fedha hizo ili nayo yaweze kustawishwa sehemu zao. Tutaendelea hivi hadi lini? Tunaambiwa kwamba tusipokuwa waangalifu, Serikali ya kitaifa itazigawa fedha hizo kwa maeneo ambayo inafikiri kwamba yanastahili kufaidika na hazina hiyo. Namuomba Mwenyekiti, kwa heshima kuu, alizingatie jambo hili ili tuhakikishe kwamba fedha hizo zimegawanyiwa maeneo yanayostahili kufaidika na hazina hiyo. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}