GET /api/v0.1/hansard/entries/561072/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 561072,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/561072/?format=api",
    "text_counter": 78,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Mhe. Naibu Spika, naomba niweke tamati nikiunga mkono ugavi wa fedha hizi. Ni matumaini yangu kwamba Mswada huu utapitishwa, na kwamba miradi inayoendelea itatekelezwa vyema na wala haitatekelezwa kiholela kama ilivyofanyika mwaka jana. Kandarasi ya kujenga barabara ya kutoka Voi kwenda Mwatate hadi Wundanyi ilitolewa lakini baadaye, Serikali ikakataa kuufadhili mradi huo na mwenye kandarasi akaondoka. Rais alipoenda Taita- Taveta hivi juzi, alisema mwenye kandarasi atarudi mwezi wa kwanza na, ghafla bin vuu, akarudi. Naomba kwamba kwenye miradi inayofadhiliwa na Serikali, kusiwe na ukora. Haki ifanywe na fedha zitumike vyema ili miradi yote ikamilike."
}